Na Christina Gauluhanga, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Ushirikiano na Maendeleo wa Serikali ya Denmark,
Charlote Slen ameishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ihakikishe misamaha
ya kodi inalenga kuwapunguzia wananchi
umaskini na kuleta usawa.
Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam
jana na Naibu Waziri Slen alipotembelea TRA nchini hapa ambapo amekuja nchini
hapa kwa ziara ya kiserikali na alifika TRA ili kufahamu mamlaka hiyo ina
mpango gani wa miaka mitano ijayokwa lengo la kupunguza umaskini Tanzania.
Alisema mfano kwa Serikali ya Denmark inahakikisha misamaha ya
kodi ni sawa kwa sawa hivyo imesaidia kupunguza umaskini kwa kutumia mbinu
mbalimbali za kisasa.
Hata hivyo Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitillya alisema
dhamira hiyo itatekelezwa kwakuwa serikali iliweka lengo hilo hivyo ana imani litatekelezeka.
Kitillya alisema tangu kuanza kutumika kwa mashine hizo
katika awamu ya kwanza wafanyabiashara 14,800 wamejiunga na mfumo huo sawa na
asilimia 92.
Alisema kutokana na mwamko huo wamehakikisha wanapata
wasambazaji wa kutosha wa mashine hizo na karatasi pamoja na kutoa mafunzo
mbalimbali kwa watendaji ili kuondoa changamoyo zikazojitokeza.
Alisema serikali ilianzisha mfumo huo Julai mwaka 2010 lwa
nego la kuboresha kumbukumbu za wafanyabiashara wanaotoza na kukusanya kodi za
Ongezeko la Thamani (VAT), ambapo awamu ya pili iliyozinduliwa jana inawahusu
wafanyabiashara ambao hawatozi VAT.
“ Awamu hii imelenga kuanza na kundi la wafanyabiashara
wapatao 200,000 wenye mauzo ghafi yenye thamani ya Sh Mil 14 kwa mwaka,”alisema
Kitillya.
Kitillya alisema tangu kuanza kutumika kwa mashine hizo kwa
miaka miwili sasa wameona mafanikio ambapo takwimu zinaonesha kuwa kwa mwaka wa
kwanza wa utekelezaji mfumo huo wamekusanya makusanyo yatokanayo an VAT
yalikuwa asilimia 9 na kufikia asilimia 23.
Naye Naibu Kamishna wa Kodi, Rished Bade alisema mashine hizo zimetengenezwa kwa
kuzingatia faida anazoweza kuzipata mtumiaji katika uendeshaji wa biashara
yake.
Alisema ili kurahisisha upatikanaji wa mashine hizo, TRA imeingia
makubaliano na kusaini mikataba na makampuni 11 ambayo yatasambaza na kutoa
elimu kwa watumiaji wa mashine hizo.
Pia kampuni nne zimeteuliwa kusambaza karatasi zenye ubora
wa kutoa risiti zisizofutika ambazo zinatumiwa na mashine hizo.
No comments:
Post a Comment