Saturday, May 18, 2013

Milipuko hatari yakamatwa Dar es salaam.



Aziza Juma na Anolina Herman, Dar es Salaam.

JESHI la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limefanya msako na kufanikiwa kuwakamata watu watano wakiwa na milipuko hatari katika msako unaoendelea jijini Dar es Salaam.  

Akizumza Kamanda wa polisi kanda maalum Dar es Salaam  Suleymani Kova alisema kuwa msako huo ulifanyika maeneo ya kunduchi na kukamata  kundi moja linalojishughulisha na maswala ya milipuko na kumiliki vifaa vya milipuko bila ya kibali kitoka Polisi. 

Alisema Kova watuhumiwa hao wametajwa kuwa ni Juma Khaluifani (24), Ruben Patrick(26),Happy Charles(28), Sadick Seif(32)na Iddi Shabani(40) wote ni wakazi wa Mtongani Jijini Dar es Salaam.

Alisema Kova watuhumiwa hao walikutwa na vifaa mbalimbali vya milipuko nyaya 62 za milipuko zikiwa zimefungwa betri,nyaya ndefu mizunguko minne ,tyubu 20 za urefu wa sentimita 30 zilizojazwa mbolea ya urea na tambi rola 1 .

“Vifaa vyote hivyo ni hatari na vikiunganishwa vinaweza kuhatarisha maisha ya watu na mali zao”,alisema Kova

Pia alisema watumiwa haohao walikutwa na dawa za kulevya aina ya bhangi gunia moja.
Alimalizia kwakusema kuwa uchunguzi zaidi unafanyika ili kujua madhumumi halisi ya watuhumiwa hao katika kumiliki vifaa saidizi na milipuko hiyo hatari.

No comments:

Post a Comment