Adelina
Rutale na Aziza Juma, Dar es Salaam
JESHI la
polisi Kanda Maalum limefanikiwa kukamata vipande 650 vya Shaba vilivyokuwa vikisafirishwa kutoka nchini Zambia
kuja bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza
jijijini Dar es Salaam jana Kamanda wa polisi Kanda Maalumu Suleiman Kova
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa katika msako huo pia
walifanikiwa kukamata meno ya tembo 27, ngozi nne za chui na fedha bandia zenye
thamani ya shilingi milioni saba.
Alisema kuwa
wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa saba ambao watafikishwa mahakamani muda
wowote ili kujibu mashitaka yanayowakabili.
“Jeshi la
polisi limefanya kazi ya msako ambapo tumeweza kuwakamata watuhumiwa hao saba
wakiwa na mali
mbalimbali kinyume na sheria,
“Tunaendelea
na uchunguzi wa kina ili kuendelea kukamata wahalifu wanaosafirisha mali za
watanzania,”alisema Kova.
Pia Kova
alisema kuwa katika msako huo walifanikiwa kukamata feni 50,bunduki moja aina
ya SMG ikiwa na namba 2608997 ikiwa na
magazine na gari aina ya SUZUKI CARRY yenye
namba za usajili T 289 BYL huko
maeneo ya Kibangulile mkoa wa Temeke.
No comments:
Post a Comment