
Wanawake hupenda kuonekana nadhifu sikuzote na katika kufanya hivyo wanatumia vitu mbalimbali vikiwamo rangi za aina mbalimbali ambazo baadhi yake hupakwa katika miili yao ikiwamo midomo.
Rangi na mafuta ya midomo ambayo hutumiwa zaidi na
wanawake yanaelezwa kuwa na sumu ambayo huweza kusababisha saratani ya
mapafu, kushindwa kwa figo kufanya kazi na hata maumivu ya tumbo.
Utafiti uliochapishwa Januari mwaka huu na Jarida
la Sayansi ya Mazingira nchini Uingereza (JES) umebaini kuwa matumizi
ya muda mrefu ya rangi za midomo na ‘lipglosses’ yanaweza kusababisha
maradhi kadhaa kutokana na kuwa na kiwango cha madini ya aluminiam,
cadmium na risasi (lead).
Kemikali zinazopatikana zaidi katika rangi za midomo zinatajwa kuwa ni cadmium, chromium, titanium, lead na manganizi.
Ingawa bidhaa hasa zenye wingi wa madini hayo
hazijawekwa wazi,wanasayansi hao wanasema kuwa ni zile zinazotumiwa au
kupendwa zaidi na kinamama.
Imebainika kuwa kupaka ‘lipshine’ au ‘lipstick’
mara tatu na zaidi kwa siku kunaweza kusababisha maradhi hayo na
ilishauriwa kuwa matumizi yake yasiwe ya muda mrefu.
Mkuu wa utafiti huu, Katharine Hammond,
mwanasayansi wa mazingira na afya katika Chuo Kikuu cha California,
Marekani anasema nia ya utafiti huo ni kutaka kupima kiwango cha
madini hayo ambacho mtumiaji wa lipstiki huweza kukimeza na kiwango
kinachokubalika.
“Kiafya, mtumiaji hatakiwi kunywa au kumeza zaidi ya asilimia
20 ya metali za lead au cadmonium hata katika maji tu ya kunywa,”
anasema Hammond
Utafiti wa Hammond unaeleza kuwa bidhaa hizo zina
kiwango kikubwa cha aluminium, cadmium, chromium na manganizi
kilichozidi asilimia 20.
Hali ikoje nchini
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na
Madawa(TFDA) Gaudensia Simwanza anasema madini ya Lead na Titanium yapo
kwenye orodha ya mchanganyiko uliozuiwa.
“Lakini madini ya titanium dioxide ndiyo yanaruhusiwa na siyo titanium zote” anasema Simwanza
source: Lipstiki--lipshine-zenye-madini-ya-sumu
No comments:
Post a Comment