Adelina Rutale na Aziza Juma, Dar es Salaam
IMEELEZWA kuwa zaidi ya asilimia 75 ya
watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi wanajihusisha na shughuli zilizopo
katika sekta isiyo rasmi ili kujipatia kipato chao.
Kauli
hiyo imetolewa baada ya kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira nchini kinazidi
kushika kasi hali ambayo imeendelea kuzitesa nchi zinazoendelea za afrika
mashariki na kusini mwa jangwa la Sahara.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Idara ya Kazi na Ajira katika Wizara
ya Kazi na Ajira Ally Msangi kwa niaba
ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Erick Shitindi katika kikao kilichowakutanisha
wadau mbalimbali kujadili hali ya soko
la ajira duniani.
Msangi
alisema kuwa utafiti huo utagusa sehemu kubwa ya nguvu kazi na utaiwezesha
serikali kupata picha halisi ya hali ya ajira nchini,utafiti huo hutoa taarifa
kuhusu hali ya ajira nchini katika sekta isiyo rasmi,utumikishwaji wa watoto,hali
ya hifadhi ya jamii,hali ya kipato nchini na matumizi ya muda na ajira mpya
zilizozalishwa katika sekta zote kwa kipindi husika (2006-2013).
“Katika
kufikia dira ya maendeleo ya taifa (vision 2025) Tanzania imejiwekea mikakati
mbalimbali ikiwemo mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini Tanzania(MKUKUTA)
wenye malengo ya kuhakikisha kiwango cha ukosefu wa ajira
kinapungua,utumikishwaji wa watoto unapungua na ajira isiyotimilifu inapungua.
“Utafiti
huu pekee wa hali ya nguvu kazi nchini ndio unaweza kutoa hali halisi ya
viashiria hivyo ili kufikia malengo na maendeleo tunayoyahitaji,”alisema
Msangi.
Alisema
kuwa kwa sasa imebaki miaka miwili kufikia hitimisho la tathmini ya malengo ya
maendeleo ya millenia (MDGs) mwaka 2015 ambapo nchi inapaswa kutoa taarifa ya
viwango vya viashiria vya malengo hayo hususani katika MDGs.
“Wote
ni wadau nuhimu katika mchakato huu kwa kuwa masuala ya ajira na kazi ni
masuala mtambuka ambayo juhudi za pamoja zinahitajika kati ya serikali,taasisi
za elimu,taasisi za utafiti,wawekezaji,mashirika yasiyo ya serikali,wabia wa
maendeleo,waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla ili kufikia malengo
tuliyojiwekea,”alisema Msangi.
No comments:
Post a Comment