
Baadhi ya vyakula vimekuwa vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti maji ni miongoni mwa vyakula hivyo. Kwanza ule mchanganyiko wa rangi zake hulifanya sio tu kuvutia bali kuwa kama ua lililochanua juu ya meza ya mlaji husika.
Kama vile haitoshi tunda hili limejaaliwa virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa katika afya ya mwanadamu.
Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado
zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana
kutofahamika kwa wengi. Zifuatazo ni baadhi tu ya faida chache kati ya
nyingi za tunda hili la tikiti maji:
Tikiti maji ni chanzo kizuri cha vitamini. Katika
tunda hilo kuna Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia
kuondosha sumu mwilini; Vitamin C, inayosaidia kuboresha kinga, kuponya
majeraha, kukinga uharifu wa seli, kuboresha afya meno na fizi; na
vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha protini
kuwa nishati.
Tunda la tikiti maji lina kiwango kikubwa cha lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani.
Ikiwa familia yako inaishi kwenye eneo lisilo na
vyanzo vya madini ya potasium, unaweza kuwapa tikiti badala yake. Lina
uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya
kazi zake vizuri.
Halikadhalika tunda hili huweza kukuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu.
Tikiti pia lina amino asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa yake.
Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili, ni ule
uwezo wake wa kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu
za kiume. Kwa kunywa juisi yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda
yake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo hilo.
Kwa kawaida tunda hili huliwa peke yake au kwa
kuchanganya na matunda mengine. Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya afya
ya vyakula kila kitu kwenye tikiti maji kina faida kiafya ukianzia
kwenye majani tunda na hata nyama yake.
source: Faida za tikitiki maji.
source: Faida za tikitiki maji.
No comments:
Post a Comment