Na Aziza Juma, Dar ea Salaam.
WAFANYABIASHARA wa vifaa vya
ujenzi wameishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupunguza bei ya mashine za
kutolea risiti ili wafanyabiashara wote kumudu kununua mashine hizo.
Akizungimza na MTANZANIA
jana mmoja wa wafanyabiashara hao
Matchowea Malisa katika semina ya wafanyabiashara inayoendelea katika wilaya ya
Temeke jijini Dar es Salaam.
Malisa alisema kuwa
wafanyabiashara wengi wanatumia mikopo kuendesha biashara zao hivyo itakuwa
vigumu kutafuta rejesho la mkopo benk wakati huhuo anatakiwa kununua mashine
ambayo inauzwa bei kubwa kiasi cha laki
nane.
Alisema pamoja mashine zina
faida kubwa na nyingi sana lakini zinafanya kazi
taratibu sana
hali inayopelekea ugumu wateja wanapokiwa zaidi ya wawili.
Pia Malisa alisema kuwa
watengenezaji wa bedhaa na wafanyabiashara wa jumla waseuza rejareja bidhaa
wanazotengeneza ili kuwapa nafasi ya wale wanaouza rejareja tu waweze kuuza
kwani wateja wote wanakimbilia huko kwakua bei yao
ya chini sana.
Aliongezea kuwa msamaha wa kodi
kwa wafanyabiashara wenyemtaji mdogo usiozidi milioni nne unapunguza uzalendo
kwani watakuwa hawana uchungu na nchi yao
pia hawato changia
ongezeko la pato la Taifa.
No comments:
Post a Comment