Adelina Rutale na Maneno Selanyika,Dar es Salaam
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam
Said Meck Sadick amewataka viongozi wa mipango miji kutokuwapimia viwanja
wananchi maeneo ya mabondeni ambayo ni hatari kwa maisha yao baada ya mafuriko kutokea.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa kuhitimisha
siku ya maadhimisho ya Mazingira Duniani Sadick alisema kuwa baadhi ya viongozi
wamekuwa wakijichukulia sheria ya kupima viwanja maeneo ya mabondeni kinyume na
sheria.
Pia alisema kuwa wananchi wamekuwa mstari wa mbele kuharibu
mazingira kwa kuchimba michanga na kokoto maeneo mbalimbali ya hapa Dar es
salaam na kusababisha adha ya mazingira kuwa machafu.
“Viongozi wa mipango miji wajitahidi kusimamia kazi yao,waache kuwapimia wananchi maeneo ya mabondeni huko
mafuriko yakitokea yanasababisha hasara kubwa ya mali
kupotea na binadamu kupoteza maisha yao,
“Watu wengi wanalalamika Dar es Salaam
kuchafu lakini waharibifu ni wao wenyewe hakuna mtu mwingine,tukiamua kuyatunza
mazingira tunaweza kuwa na sifa kama mikoa
mingine ambayo ibnasifika kwa usafi,”alisema Sadick.
Hatahivyo Sadick alisema kuwa viongozi wasimamie sheria za
kutunza kwa kutimiza wajibu wao wa uwajibikaji,taasisi kuitekeleza sheria namba
20 ya mwaka 2004 kama inavyoagiza ya kutunza
mazingira.
“Watendaji kupanga matumizi ya ardhi kwa uadilifu kulingana
na sifa za ardhi husika mfano kutoruhusu ujenzi mabondeni,ufukweni na utengaji
wa maeneo kwa shughuli mbalimbali za kijamii,
“Wananchi kutokupenda kutii sheria zilizopo kwa hiari bila
shuruti,usimamizi hafifu na usioridhisha wa sheria ndogondogo na hifadhi ya
mazingira,”alisema Sadick.
Pia alisema kuwa kila mwananchi wa mkoa huu watafakari kwa
kina juu ya shughuli za uzalishaji wa kiuchumi zunazozingatia utunzaji wa
mazingira kwani ni muhimu kuwa na mazingira endelevu kama
nchi nyingine.
Aidha viongozi mbalimbali walihudhulia kwenye siku hiyo
ikiwemo mkuu wa wilaya,wakurugenzi,madiwani,wenyeviti na wadau mbalimbali
kutoka asasi zisizo za kiserikali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtandao wa uthibiti wa
mabadiliko ya tabia ya nchi (FOFUM CC), Euster Kibona, alisema wamejitahidi
kufanyakazi na jamii nzima hasa katika maeneo ya mijini na vijijini kufanya
shughuli za uzalishaji kwa maendeleo endelevu bila kuathiri mazingira.
Alisema kuwa maeneo ya miji ambako kuna viwanda vingi ndiko
kunakoonekana kuathirika zaidi na uchafuzi wa mazingira kutokana na hewa
inayotoka viwandani, maji machafu na taka nyingine nyingi.
“Kulinda na kutunza mazingira ni jukumu la mimi wewe na sisi
hivyo tunatakiwa kila mmoja kuchukua hatua kuanzia sasa ili kuondokana na
maginjwa yasiyotarajiwa kama vile ya mlipuko
na mengine,” alisema Kibona.
No comments:
Post a Comment