Na Aziza Juma, Dar es Salaam.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajia kuanza
mkakati wa kuwazungukia wafanyabiashara katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar
es Salaam lengo likiwa ni kutoa elimu juu ya matumizi ya mashine ya kutolea
risiti.
Akizungumza na MTANZANIA jana
Afisa mwandamizi wa elimu wa TRA Hamisi Lupenja ziara hiyo itaanza baada ya kumaliza
semina inayoendelea kwa wafanyabiashara
hao.
Lupenja alisema mafunzo haya
yanawalenga wale wafanyabiashara wenye pato la zaidi ya milioni 14 kwa mwaka na
hasa wafanyabiashara ya vifaa vya ujenzi, nguo, vipuri, baa na hoteli.
“Mafunzo hayo ni kwajili ya
faida kwa wafanyabiashara sio kwa TRA tu kwani inasaidia kutunza kumbukumbu za mauzo na kudhibiti ubabaishaji
wa wasaidizi wao hata wakisafiri” alisema Lupenja.
Kwaupande wake mfanyabiashara
wa vipuri Hanifa Adam aliipongeza TRA kwa
hatua waliyoifanya kwani imewajengea uwelewa wa kutosha juu ya matumizi ya
mashine hizo.
“Tunaishukuru TRA kwa mafunzo
haya kwani yametusaidia sana
katika kutumia na kujua umuhimu wa mshine hizi” alisema Hanifa.
No comments:
Post a Comment