Aziza Juma na Vick Kanje ,Dar
es Saalam
AFISA mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA )Hamisi Lupenja
amewataka wawekezaji kutoka Nchi ya China kupewa
elimu ya uwekezaji wa majengo na ujenzi.
Akizungumza katika semina
hiyo jana jijini Dar es Saalm, Lupenja alisema kuwa lengo la kutoa semina hiyo ni
kutoa elimu kwa wawekezaji wa majengo na ujenzi na pia kuboresha mfumo wa kodi.
‘Tupo na jamii ya Wachina
tunawapa elimu kuhusu kodi katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya upangishaji
na kufuata sheria za nchi.
‘Jukumu letu la msingi ni
kuwapa elimu ili kuwawezesha kufanya biashara zao kwa ufanisi zaidi ’alisema
Lupenja.
Lupenja alisema kuwa
wameshafanya semina nyingi na sehemu mbalimbali ikiwemo semina kutumia machine
ya Electronic kwa wafanyabiashara .
Alisema kuwa wapotayari
kukumbana na changamoto wakati wa utoaji elimu kwa wafanyabiashara na kuna
baadhi ya wafanyabiashara wanaojua kutumia mashine hizo lakini wanakuwa wabishi
kutumia wakidai hawajui jinsi ya kutumia .
MWISHO.
Hata hivyo alisema kuwa
wanatoa elimu kwa wafanyabiashara wote bila kujali ni Mchina au Mtanzania.
No comments:
Post a Comment