Wednesday, September 19, 2012

17 MBARONI KWA BIASHARA HARAMU YA BHANGI NA GONGO



JESHI la polisi mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam limewatia mbaroni watuhumiwa 17  kwakosa la kufanya biashara haramu  ya  bhangi na pombe ya aina ya gongo .

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo  Kamanda wa Polisi  Mkoa Kinondoni Charles Kenyela aliwataja watuhumiwa  hao ni Jonathan Johsoni{ 26 } ,Mashaka Salehe {32}, Ramadhni Abubakari {21}, Paazi Chemba(21),Tajiri Saumani(32), Inocent Riberty(28),Agnes Andrew(20) na wenzao kumi wote wakazi wa Dar es Salaam.

Alisema Kenyela kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika msako maalumu wa polisi  maeneo ya Kigogo,Magomeni, Manzese na Mburahati, wakiwa na bhangi debe nane na kete 152 pamoja lita 15 za pombe haramu aina ya Gongo.

Wakati huohuo  watuhuhiwa watano wanashikiliwa na jeshi la Polisi mkoa wa Temeke kwa tuhuma za kukutwa na puri tano na misokoto 21 ya bhangi pamoja na  lita sita za  pombe haramu aina ya Gongo.

Akithibisha  kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke David Misime  aliwataja watuhumiwa hao ni Mchawa Ibrahim(51), Ami Musa(22), Athuman  Abdalah (18),Halima  Juma(24) na Lusekelo  William(18) wote wakazi wa Mtongani Kichanga jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment