Saturday, May 18, 2013

Milipuko hatari yakamatwa Dar es salaam.



Aziza Juma na Anolina Herman, Dar es Salaam.

JESHI la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limefanya msako na kufanikiwa kuwakamata watu watano wakiwa na milipuko hatari katika msako unaoendelea jijini Dar es Salaam.  

Akizumza Kamanda wa polisi kanda maalum Dar es Salaam  Suleymani Kova alisema kuwa msako huo ulifanyika maeneo ya kunduchi na kukamata  kundi moja linalojishughulisha na maswala ya milipuko na kumiliki vifaa vya milipuko bila ya kibali kitoka Polisi. 

Alisema Kova watuhumiwa hao wametajwa kuwa ni Juma Khaluifani (24), Ruben Patrick(26),Happy Charles(28), Sadick Seif(32)na Iddi Shabani(40) wote ni wakazi wa Mtongani Jijini Dar es Salaam.

Alisema Kova watuhumiwa hao walikutwa na vifaa mbalimbali vya milipuko nyaya 62 za milipuko zikiwa zimefungwa betri,nyaya ndefu mizunguko minne ,tyubu 20 za urefu wa sentimita 30 zilizojazwa mbolea ya urea na tambi rola 1 .

“Vifaa vyote hivyo ni hatari na vikiunganishwa vinaweza kuhatarisha maisha ya watu na mali zao”,alisema Kova

Pia alisema watumiwa haohao walikutwa na dawa za kulevya aina ya bhangi gunia moja.
Alimalizia kwakusema kuwa uchunguzi zaidi unafanyika ili kujua madhumumi halisi ya watuhumiwa hao katika kumiliki vifaa saidizi na milipuko hiyo hatari.

Wizara ya Maji inahitaji Sh.bilion 4.6 kusomesha wataalamu wa maji.


Ruth Mnkeni na Aziza Juma, Dar es Salaam.

JUMLA ya Sh.bilioni 4.6 zinahitajika  kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi wa walio vyuoni ili kuboresha maendeleo katika sekta ya maji nchini.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe wakati wa kuzindua Mfuko wa Udhamini wa Maji (WTF)  ambao unawasomesha wanafunzi wanaochukua taaluma ya sekta ya maji.

Profesa Maghembe alisema kuwa mfuko huo utasaidia kuboresha sekta hiyo kwani mahitaji ya maji ni makubwa katika maisha ya binadamu.

Aliongeza kusema kuwa wanao mpango mkakati wa kusambaza maji katika maeneo ya vijijini kwani kuna vyanzo vingi ijapokuwa vinaathiriwa na watu wachache kwa manufaa yao binafsi .

“Kuna watu ambao ni wezi wa maji wanajitengenezea visima wakidai kuwa vinatoa maji kumbe wanatumia maji ya DAWASCO lakini tulifanya operesheni ya miezi mwili na tuliwakamata zaidi ya watu 90 ambao walikuwa wanaiba maji,”alisema

“Juhudi hizi zimepelekea sehemu nyingi katika jiji la Dar es Salaam kupata maji tofauti na ilivyokuwa awali kwani baadhi yao wamehukumiwa na wengine kesi zinaendelea katika mahakama ya jiji .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mfuko huo Dayana Mwiru alisema lengo la kuanzisha mfuko huo ni kujaribu kuongeza idadi ya wanataaluma wa sekta ya maji kwani ni wachache mno.

Alisema utafiti uliofanywa mwaka 2011 ulionyesha kuwa mahitaji ya maji yanahitaji wanataaluma 3000 ili kuweza kufanya kazi ipasavyo tofauti na sasa ambapo haikidhi kwani kuna chuo kimoja tu kinachotoa taaluma hiyo na kwa sasa kuna wanafunzi 1600 ambao wapo kwenye taaluma hiyo.

“Mfuko huu utasaidia kwenya idadi ya wanafunzi kwa kuangalia usawa wa jinsia, watu wanaotoka katika familia duni na pia  wanawake kuwapa kipaumbele ili kuhakikisha kuwa wanafikia malengo bila kujali anatoka katika falimilia gani,”alisema Mwiru.

75% ya watanzania wajihusisha na shughuli zilizo katika sekta isiyo rasmi.

 Adelina Rutale na Aziza Juma, Dar es Salaam
 IMEELEZWA kuwa zaidi ya asilimia 75 ya watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi wanajihusisha na shughuli zilizopo katika sekta isiyo rasmi ili kujipatia kipato chao.

Kauli hiyo imetolewa baada ya kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira nchini kinazidi kushika kasi hali ambayo imeendelea kuzitesa nchi zinazoendelea za afrika mashariki na kusini mwa jangwa la Sahara.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana  Mkurugenzi wa Idara ya Kazi na Ajira katika Wizara ya  Kazi na Ajira Ally Msangi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Erick Shitindi katika kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali  kujadili hali ya soko la ajira duniani.

Msangi alisema kuwa utafiti huo utagusa sehemu kubwa ya nguvu kazi na utaiwezesha serikali kupata picha halisi ya hali ya ajira nchini,utafiti huo hutoa taarifa kuhusu hali ya ajira nchini katika sekta isiyo rasmi,utumikishwaji wa watoto,hali ya hifadhi ya jamii,hali ya kipato nchini na matumizi ya muda na ajira mpya zilizozalishwa katika sekta zote kwa kipindi husika (2006-2013).

“Katika kufikia dira ya maendeleo ya taifa (vision 2025) Tanzania imejiwekea mikakati mbalimbali ikiwemo mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini Tanzania(MKUKUTA) wenye malengo ya kuhakikisha kiwango cha ukosefu wa ajira kinapungua,utumikishwaji wa watoto unapungua na ajira isiyotimilifu inapungua.

“Utafiti huu pekee wa hali ya nguvu kazi nchini ndio unaweza kutoa hali halisi ya viashiria hivyo ili kufikia malengo na maendeleo tunayoyahitaji,”alisema Msangi.

Alisema kuwa kwa sasa imebaki miaka miwili kufikia hitimisho la tathmini ya malengo ya maendeleo ya millenia (MDGs) mwaka 2015 ambapo nchi inapaswa kutoa taarifa ya viwango vya viashiria vya malengo hayo hususani katika MDGs.
“Wote ni wadau nuhimu katika mchakato huu kwa kuwa masuala ya ajira na kazi ni masuala mtambuka ambayo juhudi za pamoja zinahitajika kati ya serikali,taasisi za elimu,taasisi za utafiti,wawekezaji,mashirika yasiyo ya serikali,wabia wa maendeleo,waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla ili kufikia malengo tuliyojiwekea,”alisema Msangi.

Waziri Charlote Slen wa Denmark aishauri TRA kuhusu misamaha ya kodi.


Na Christina Gauluhanga, Dar es Salaam

NAIBU Waziri wa Ushirikiano na Maendeleo wa Serikali ya Denmark, Charlote Slen ameishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ihakikishe misamaha ya kodi inalenga  kuwapunguzia wananchi umaskini na kuleta usawa.

Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam jana na Naibu Waziri Slen alipotembelea TRA nchini hapa ambapo amekuja nchini hapa kwa ziara ya kiserikali na alifika TRA ili kufahamu mamlaka hiyo ina mpango gani wa miaka mitano ijayokwa lengo la kupunguza umaskini Tanzania.

Alisema mfano kwa Serikali ya Denmark inahakikisha misamaha ya kodi ni sawa kwa sawa hivyo imesaidia kupunguza umaskini kwa kutumia mbinu mbalimbali za kisasa.

Hata hivyo Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitillya alisema dhamira hiyo itatekelezwa kwakuwa serikali iliweka lengo hilo hivyo ana imani litatekelezeka.

Kitillya alisema tangu kuanza kutumika kwa mashine hizo katika awamu ya kwanza wafanyabiashara 14,800 wamejiunga na mfumo huo sawa na asilimia 92.

Alisema kutokana na mwamko huo wamehakikisha wanapata wasambazaji wa kutosha wa mashine hizo na karatasi pamoja na kutoa mafunzo mbalimbali kwa watendaji ili kuondoa changamoyo zikazojitokeza.

Alisema serikali ilianzisha mfumo huo Julai mwaka 2010 lwa nego la kuboresha kumbukumbu za wafanyabiashara wanaotoza na kukusanya kodi za Ongezeko la Thamani (VAT), ambapo awamu ya pili iliyozinduliwa jana inawahusu wafanyabiashara ambao hawatozi VAT.

“ Awamu hii imelenga kuanza na kundi la wafanyabiashara wapatao 200,000 wenye mauzo ghafi yenye thamani ya Sh Mil 14 kwa mwaka,”alisema Kitillya.

Kitillya alisema tangu kuanza kutumika kwa mashine hizo kwa miaka miwili sasa wameona mafanikio ambapo takwimu zinaonesha kuwa kwa mwaka wa kwanza wa utekelezaji mfumo huo wamekusanya makusanyo yatokanayo an VAT yalikuwa asilimia 9 na kufikia asilimia 23.

Naye Naibu Kamishna wa Kodi, Rished Bade  alisema mashine hizo zimetengenezwa kwa kuzingatia faida anazoweza kuzipata mtumiaji katika uendeshaji wa biashara yake.

Alisema ili kurahisisha upatikanaji wa mashine hizo, TRA imeingia makubaliano na kusaini mikataba na makampuni 11 ambayo yatasambaza na kutoa elimu kwa watumiaji wa mashine hizo.

Pia kampuni nne zimeteuliwa kusambaza karatasi zenye ubora wa kutoa risiti zisizofutika ambazo zinatumiwa na mashine hizo.

Jeshi la Polisi laokoa shaba ikiwa inatoroshwa.


Adelina Rutale na Aziza Juma, Dar es Salaam
JESHI la polisi Kanda Maalum limefanikiwa kukamata vipande 650 vya Shaba vilivyokuwa vikisafirishwa kutoka nchini Zambia kuja bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza jijijini Dar es Salaam jana Kamanda wa polisi Kanda Maalumu Suleiman Kova alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa katika msako huo pia walifanikiwa kukamata meno ya tembo 27,  ngozi nne za chui na fedha bandia zenye thamani ya shilingi milioni saba.

Alisema kuwa wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa saba ambao watafikishwa mahakamani muda wowote ili kujibu mashitaka yanayowakabili.

“Jeshi la polisi limefanya kazi ya msako ambapo tumeweza kuwakamata watuhumiwa hao saba wakiwa na mali mbalimbali kinyume na sheria,

“Tunaendelea na uchunguzi wa kina ili kuendelea kukamata wahalifu wanaosafirisha mali za watanzania,”alisema Kova.

Pia Kova alisema kuwa katika msako huo walifanikiwa kukamata feni 50,bunduki moja aina ya SMG ikiwa na namba  2608997 ikiwa na magazine na gari aina ya SUZUKI CARRY yenye  namba za usajili  T 289 BYL huko maeneo ya Kibangulile mkoa wa Temeke.

Monday, March 11, 2013

Woman needs 4 organs to survive

Molly Pearce has had what her mother dryly calls "a very alternative life" since birth because of her chronic health issues.
The 24-year-old Santa Monica, California, woman has Hirschsprung's disease, a rare congenital disorder that obstructs the large intestine due to an absence of nerve cells that regulate muscle movement.
She never attended public school full time, has been in and out of hospitals since she was a newborn, and discovered that the one thing she can eat without getting sick is a bag of Cheetos.
Now, Pearce needs four organs -- a liver, kidney, pancreas and small intestine -- from a deceased type O donor to live.
"It's a pretty unusual circumstance," said Dr. Alan Langnas, chief of transplantation at the University of Nebraska Medical Center, where Pearce is being treated. "Fortunately, she's young, and youth trumps everything. She's in very good shape relative to her condition."
At birth, Pearce was one of only three people in the world with her particular type of disease, and doctors predicted she wouldn't live beyond her first year.
Growing up, "I would go to school when I could, but I didn't know anybody and always felt left out," Pearce said. "Most of the time I felt OK, but I was really in a fragile state. I just wanted to be a normal kid."
Pearce managed her disease as well as possible but experienced a major setback at 12 when she was given a drug too powerful for someone of her size. It destroyed her small intestine and her kidney, forcing her onto a liquid diet. It wasn't until she was 17 that she received a small intestine transplant, and at 18 she accepted one of her mother's kidneys.