Monday, September 16, 2013
Friday, September 6, 2013
Mikopo kwa wajasilia mali inakuza mitaji na biashara.
Na Aziza Juma, Dar es Salaam.
MUWAKILISHI wa vikundi vya wajasiriamali wanawake, Inuka, David Msuya, amesema akiba anayojiwekea mjasiriamali inaweza kuinua na kuendeleza mtaji wake ikiwa walengwa watatambua fursa hiyo na kuitumia kikamilifu.
Msuya alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam juzi wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali wa kata ya Manzese.
Alisema wanawake wengi hawajui jinsi ya kutumia mikopo kujiajili na kufanya biashara, hivyo kuwataka wajiamini na kufanya biashara bila utegemezi katika kuendesha maisha yao.
“Wanawake wajasiriamali ni msaada mkubwa katika familia; wanatakiwa kuamka ili kuendesha maisha yao bila ya kuwa tegemezi.“Tunatoa mikopo kwa kinamama wajasiriamali kati ya sh milioni 6 had sh milioni 25, ili kuwawezesha kufanya biashara,” alisema Msuya.Hata hivyo alisema mkopo wa sh milioni 25 ni kwa ajili ya wafanyakazi, ili kuwawezesha kukarabati nyumba zao na kuendesha biashara.

Subscribe to:
Posts (Atom)